Mshambuliaji Okwi katika mchezo uliopita dhidi ya Saoura alifunga bao na kutegeneza mawili hivyo kukosekana kwake ni pigo kwa mabingwa wanaotaka ushindi ili kusonga mbele kwa robo fainali.
Okwi alikosekana katika mechi iliyopita ya Ligi Kuu Bara Simba ikishinda 2-0 dhidi ya Stand United bila ya kuweka wazi sababu ya nyota huyo kukosekana.
Alipotafutwa kocha msaidizi wa Simba, Denis Kitambi kuhusu kukosekana kwa Okwi alisema kwa kifupi siwezi kulizungumzia hilo kwa sasa.
Akizungumzia kuondoka kwa Simba bila ya Okwi, nahodha Bocco alisema hata kama kuna baadhi ya mchezaji anakosekana bado malengo yao ya kufanya vizuri yapo pale pale.
Alisema hilo la kukosekana kwa baadhi ya wachezaji halipo chini yangu kwani ninaimani kila mchezaji ambaye atapata nafasi ya kucheza atatimiza majukumu yake.
"Kwetu wachezaji tumepata muda wa kujiandaa vizuri na kwenda kushindana katika mechi na JS Saoura malengo yetu yakiwa ni palepale kufanya vizuri," alisema Bocco.
"Tunafahamu tunakwenda kucheza na timu ambayo itakuwa imebadilika na si ile ambayo tulicheza nayo katika mechi ya kwanza hapa nyumbani.
"Wachezaji wote waliokuwepo wanamorali ya hali ya just kubwa tunaomba Watanzania watuombee ili twende kulifanya na kulitimiza lile ambalo lipo katika mioyo yetu," alisema Bocco.
Wachezaji 20, waliondoka ni Aishi Manula, Zana Coulibaly, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Mohammed Hussein, Pascal Wawa, Poul Bukaba, James Kotei, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, Cletus Chama, Rashid Juma, Abdul Selemani, Bocco, Maddie Kagere, Adam Salamba.
Wengine Deo Munishi, Asante Kwasi, Mohammed Ibrahim na kiungo fundi Haruna Niyonzima.
ILIKUWA HIVI
Saa 7:30 mchana Mjumbe wa Bodi, Mwina Kaduguda alikuwa wa kwanza kufika uwanja wa ndege.
Dakika 15, mbele alifika Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori ambaye alikuwa amevalia suruali ya jinsi ya bluu, sweta jepesi rangi nyeusi na koti ya suti rangi ya blush huku akiwa na begi lake la kuburuza.
Saa 8:00 mchana gari ndogo ya kubebea wachezaji wa Simba 'Hiace' ilifika huku waandishi wa habari walilikumbilia kupata picha. Lakini gari hiyo ilikuja bila ya wachezaji bali walikuwepo daktari Yassin Gembe, Mtunza vifaa Hamis Mtambo, Meneja Patrick Rweyemamu, Mpishi Samuel Cyprian pamoja na mabeki ya wachezaji.
Saa 8:17 mchana kikosi cha Simba kiliwasili uwanja wa ndege na basi kwanza kushuka alikuwa Patrick Aussems na aliyefuata ni kocha msaidizi Denis Kitambi.
Baada ya hapo wachezaji hawakushuka na walikaa kwenye gari zaidi ya dakika 20, ndio walishuka na a kwanza kushuka alikuwa ni kiungo Mzamiru Yassin.
0 Comments