Salamba amefichua hilo kuwa jambo kubwa analoambia na kocha Aussems ni namna ya kufikia ndoto zake akitaka ajifunze dhidi kwa Meddie Kagere, John Bocco na Emmanuel Okwi.
"Kocha Aussems huwa ananiambia ameona kitu kwenye mguu wangu, amekuwa akinitaka nikionyesha na huwa ananiambia nicheze bila presha ili nifikie kila anachokitaka kwangu.
"Pia anasema niwatazame kina Kagere, Okwi na Bocco wanachokifanya, lakini mimi nifanye zaidi, hata zile dakika ananipa kucheza baada ya mchezo ananiita na kunielekeza nimekosea wapi na nimefanya vizuri sehemu gani.
"Kuhusu kocha Zrane amekuwa akitoa muda wake kuhakikisha ananiongoza kwa kufanya mazoezi ya kujijengea ufiti na ananiambia kuna kitu amekiona nikifanikiwa kukitoa nitakuwa mchezaji mzuri.
"Hiyo ndio sababu nikifunga nakimbilia kumlaki na amekuwa akifurahi sana nikifunga," anasema Salamba.
0 Comments