MAMA-mtoto wa rapa Travis Scott, ‘ Kylie Jenner’, amekuwa bilionea mwenye umri mdogo zaidi duniani, kwa mujibu wa orodha ya mabilionea ya gazeti la Forbes.
Kylie ambaye ni Mmarekani, ndiye mdogo zaidi katika familia ya Kardashian, amepata utajiri wake kutokana na biashara ya vipodozi.
Akiwa na umri wa miaka 20 alianzisha na anamiliki kampuni ya vipodozi ya Kylie Cosmetics, biashara ya urembo ambayo imedumu kwa miaka mitatu sasa na kuingiza mapato ya takriban Dola milioni 360 (Sh. bil. 850) mwaka jana.
Alifikia mafanikio haya mapema kuliko muasisi wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg ambaye alikuwa bilionea akiwa na umri wa miaka 23.
“Sikutarajia chochote. Sikujua hali ya baadaye. Lakini kutambuliwa inafurahisha. Ni jambo zuri la kunitia moyo,” Bi Jenner aliliambia jarida la Forbes.
Orodha ya Forbes inaonyesha muasisi wa Amazon ni Jeff Bezos, akiendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwa binadamu tajiri zaidi duniani.
Jumla ya utajiri wake ni Dola bilioni 131 kulingana na jarida la Forbes, ambapo ameongeza hadi Dola bilioni 19 kutoka mwaka 2018.
Lakini kiwango cha mapato ya mabilionea wote kwa ujumla kimeshuka kwa Dola trilioni 9.1
Miongoni mwa mabilionea ambao utajiri wao unapungua ni muanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg.
Utajiri wao umeshuka kwa Dola bilioni 8.7 na katika kipindi cha mwaka uliopita ulishuka kwa Dola bilioni 62, kwa mujibu wa orodha ya jarida la Forbes
0 Comments