Windows

MGUNDA: SERENGETI BOYS WANA MOTO, WAPO TAYARI KWA AFCON


KOCHA Mkuu wa kikosi cha timu ya Vijana chini ya miaka 20 (U 20) Ngorongoro Heroes, Juma Mgunda amesema kuwa uwezo wa kikosi cha U 17, Serengeti Boys ni mzuri na wapo kamili kwa ajili ya michuano ya Afrika kwa vijana (Afcon U 17) itakayopigwa mwezi ujao hapa nchini.

Serengeti Boys ambayo kwa sasa ipo nchini Rwanda kwa ajili ya kushiriki mashindano maalumu kwa ajili ya kujiaandaa na Afcon, walipoteza mabao 6-2 mbele ya Ngorongoro kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa JMK Park.

Mgunda amesema " Timu ipo vizuri, bila shaka wataonyesha ushindani mkubwa kwenye mashindano ya Afcon, mapungufu yao sio makubwa hivyo wana nafasi ya kufanya vizuri na kupata matokeo chanya.

"Tutakaa sisi walimu wa timu za vijana kufanyia kazi mapungufu ambayo tumeyaona ili kuviimarisha vikosi vyetu kabla ya mashindano," amesema Mgunda.

Post a Comment

0 Comments