Windows

MBAO YAPANIA KUIVURUGA SIMBA UWANJA WA JAMHURI, MIKAKATI YAO BALAA


MBAO FC waliitungua Simba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, wamepania kuivuruga Simba kwenye mchezo wao wa Jumapili utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Mbao kwa sasa ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 30 ikiwa imejikusanyia pointi 36 itamenyana na Simba ambayo ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo 21 ikiwa na pointi 54.

Kocha Mkuu wa Mbao, Salum Mayanga amesema "Tunajua tunakwenda kukutana na timu ya aina gani hivyo hatuna mashaka lazima tutapambana kutafuta matokeo uwanjani, tuna mipango mikali.

"Maandalizi yetu yamekamilika hivyo kilichobaki kwa sasa ni kuona namna gani mchezo utakuwa ndani ya dakika 90 ambazo zitaamua matokeo, mashabiki wajitokeze kutupa sapoti," amesema Mayanga.

Post a Comment

0 Comments