Lionel Messi alifunga mabao mawili katika kipindi cha pili, ikiwa ni pamoja na freekick yenye ufundi wa juu, wakati Barcelona ikiiduwaza Espanyol kwa kuifunga 2 – 0 na kuhifadhi mwanya wao wa pointi 10 kileleni mwa La Liga.
Messi amefunga mabao 22 katika mechi zake 15 za mwisho za La Liga, wakati pia amepitisha mabao 40 katika msimu mmoja kwa mara ya tano mfululizo. Amefunga mabao 31 kwenye ligi msimu huu. Nambari mbili kwenye lig Atletico Madrid waliwakaanga Alaves 4-0 katika mechi nyingine ya Jumamosi.
Saul Niguez na Diego Costa walifunga katika kipindi cha kwanza na Alvaro Morata na Thomas Partey wakaongeza mengine mawili katika kipindi cha pili na kuwapa vijana hao wa Diego Simeone ushindi mwepesi
0 Comments