Windows

Man City warejea kileleni, United yakamata nafasi ya nne

Manchester City ilirejea kwa kishindo kileleni mwa ligi baada ya kuwazika Fulham katika kichapo chao cha nane mfululizo. Vijana hao wa Pep Guardiola waliifunga Fulham 2-0 na kurejesha umahiri wao kupitia mabao ya Bernado Silva na Sergio Aguero.

Silva alifumania nyavu katika dakika ya tano ya mchezo kwa kusukuma kombora kutoka yadi 20. City ambao walikuwa na shuti 10 katika dakika 15 za kwanza, waliongeza la pili wakati Aguero alimvisha kanzu safi kipa wa Fulham Sergio Rico.

Fulham wamefungwa mabao 72 mpaka sasa msimu huu, rekodi mbaya kabisa katika Ligi ya Premier.

Guardiola na vijana wake ambao wanawinda mataji manne msimu huu, sasa wanaongoza ligi na pengo la pointi moja dhidi ya Liverpool ambao watachuana na Tottenham Jumapili.

United yakamata nafasi ya nne

Ole Gunnar Solskjaer amesema Manchester United walionekana kana kwamba wako likizo wakati uongozi wake kama kocha wa kudumu ukianza kwa ushindi wa jasho dhidi ya Watford.

Ushindi huo wa 2 – 1 ulionekana kuwa mkali kwa wageni Watford ambao waliutawala mchezo kwa kipindi kirefu na kuwa na nafasi nzuri za kufunga, lakini unaisogeza United katika nafasi ya nne juu ya Arsenal, ambao watacheza Jumatatu. Mabao ya United yalifungwa na Marcus Rashford na Anthony Martial. Abdoulaye Doucoure aliifungia Watford bao la dakika za mwisho mwisho

 

 


Post a Comment

0 Comments