Timu ya Biashara United inayopambana kuhakikisha haishuki daraja kutoka ligi kuu kwenda daraja la kwanza leo imefanikiwa kuchukua points zote tatu ikicheza na Ndanda ya Mtwara.
Biashara United ikicheza katika uwanja wake wa Nyumbani uwanja wa Kambukumbu ya Karume imepata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri yote yakipatikana kipindi cha pili.
Goli la kwanza la Biashara United limefungwa na Tariq Kiakala dakika ya 51 huku bao la pili likifungwa na George Makang’a dakika ya 58.
0 Comments