Windows

MASHAHIDI WAZUA JAMBO MAHAKAMANI, KESI YA MALINZI YASHINDWA KUSIKILIZWA




Mahakama  imeshindwa kuendelea na kesi inayowakabili  waliokuwa viongozi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kushindwa kuleta mashahidi huku wakili wake akishindwa kufika mahakamani.

Kesi hiyo ilitarajiwa kuendelea kusikilizwa kwa kuendelea kutoa ushahidi ambapo awali tayari mashahidi 11 wametoa ushahidi wao.

Wakili wa serikali, Imani Nitume ambaye alimwakilisha Leonard Swai aliiambia mahakama wakili Swai alishindwa kufika kutokana na kuwa na majukumu mengine.

Wakili huyo aliiambia mahakama kuwa kutokana na Swai kutokuwepo na ni wakili ambaye pia anaanda mashahidi ndiyo maana wameshindwa kuja na shahidi ingawa shahidi  ambaye alitakiwa kuja  naye aliomba udhuru.

Aidha  Wakili ambaye aliwawakilisha washitaki wote watano, Kashindye Thabiti aliiambia mahakama kuwa upande wa serikali unapaswa kuhakikisha kuwa unaleta mashahidi hata watatu katika kesi ijayo.

Na aliongeza kuwa kesi hiyo upande wa Takukuru wanatakiwa kutuma wawakilishi wao sababu wapo wengi na hata kama Swai asipokuwepo yupo Kimaro ambaye amekuwepo tangu awali kesi hiyo ilipoanza au mawakili wao wengine.

Hakima  Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Maira Kasonde alisema kesi hiyo imehairishwa mpaka Machi, 26/mwaka huu na serikali inatakiwa kuleta mashahidi kuweza sikiliza kesi hiyo.


Ikumbukwe Malinzi na wenzake Celestine Mwesigwa ambaye alikuwa katibu wa TFF na Mhasibu Nsiande Mwanga wakikabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha Dola za Marekani, 173,335.Na wako mahabusu kwa sababu mashtaka yao hayana dhamana kisheria

Post a Comment

0 Comments