KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kwa bongo anavutiwa na uwezo wa wachezaji watatu ambao wanacheza ndani ya Simba kutokana na uwezo ambao wanaonyesha wakiwa ndani ya Uwanja.
Zahera amesema uwezo wa mchezaji Uwanjani sio kukimbia na mpira bali ni namna ya umiliki, akili ya kutumia mpira pamoja na kuitafuta wakati mchezaji akiwa hana mpira.
"Wachezaji wengi nawafuatilia na kuangalia namna ambavyo wanacheza hasa wakiwa Uwanjani ukiaachana na wale nilionao kwenye timu yangu, kuna hawa wachezaji watatu ambao wapo Simba wananifurahisha wakiwa Uwanjani.
"John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi ni aina ya wachezaji ambao wanahitajika kwenye timu zetu ili kuongeza ushindani, kutokana na vile ambavyo wanafanya wakiwa Uwanjani, wana spidi na akili ya mpira ila sina mpango wa kuwasajili ndani ya Yanga kwa kuwa nitawaumiza watu wa Simba," amesema Zahera.
Zahera ameendelea kuwasisitiza wanachama na wapenzi wa Yanga kuendelea kuichangia timu ili kufikia malengo kutokana na kupitia kipindi cha mpito hivyo anaamini kama kila mmoja atatoa mchango kwa moyo watafanya usajili makini kwani anawatambua wachezaji wengi wenye uwezo na hawahitaji gharama kubwa.
0 Comments