Windows

LIPULI YA MATOLA YAIPIGA MKWARA MZITO YANGA


KOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amesema amejipanga kutibua mipango ya Yanga  kwa kuwa anawatambua vizuri wapinzani wake.

Yanga itashuka Uwajani Jumamosi huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza wa ligi waliocheza Uwanja wa Taifa kwa kupigwa bao 1-0.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema amepata mbinu za kuimaliza Yanga kwenye mchezo wao utakaochezwa Uwanja wa Samora.

"Tupo imara na tuna nguvu ya kusonga mbele baada ya kupata ushindi mbele ya Mbao kinachofuata kwa sasa  ni kubeba pointi zetu kwa Yanga.

"Kila kitu kinawezekana na nimeawambia wachezaji namna bora ya kufanya kuibuka kidedea kwenye mchezo wetu tutakaokuwa nyumbani," amesema Matola.

Post a Comment

0 Comments