England. Hii sasa ishakuwa shida. Ndivyo unavyoweza kuelezea kwa ufupi baada ya Manchester City kuwapa raha mashabiki wake ikishinda mabao 7-0 dhidi ya Schalke na kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulauya.
Licha ya kuangushiwa kipigo kikali, Schalke walikuwa kwenye mchezo kwa dakika zote walipokuwa uwanjani.
Leroy Sane ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo baada ya kuonyesha kiwango safi kwenye mchezo huo wa kuvutia.
Kwa ushindi huo, Manchester City imetinga robo fainali kwa kishindo kwa jumla ya mabao 10-2.
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola alisema ushindi huo mnono umetokana na uimara wa kikosi chake.
Kocha wa Schalke, Tedesco alizungumzia kipigoi hicho akionyesha kuumizwa na matokeo hayo huku akiwaomba radhi mashabiki kwa kile kilichotokea.
Manchester City imeungana na timu za Juventus, Ajax, Porto na Tottenham Hotspur kwenye hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Leo Jumatano usiku itapigwa michezo mingine ambapo Liverpool wataonyesha umwamba na Bayern Munich na Barcelona watawakaribisha Lyon.
0 Comments