Windows

KMC: HAKITAELEWEKA MPAKA TUBEBE KOMBE, WAANDAA KABATI MAALUMU


MSHAMBULIAJI wa KMC, Mohamed Rashid amesema kuwa ushirikiano mkubwa uliopo ndani ya KMC unamfanya azidi kupambana na kufanya kazi kwa juhudi zaid kila siku.

Mo Rashid alitimiza majukumu yake ipasavyo kwenye Uwanja wa Isamuhyo Juzi baada ya kuanza kuifungia moja ya bao kwenye  ushindi wao wa mabao 2-0 na kufikisha bao lake la tatu FA, hali iliyowafanya watinge hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho.

"Tunapambana kwa pamoja kila mmoja anapenda kuona timu inapata matokeo, hizo ndio hesabu zetu ndani ya timu na kikubwa ambacho kinatufanya tushinde ni umoja wetu na mbinu za mwalimu.

"Tumeandaa kabati maalumu kwa ajili ya kuweka kombe la FA kwa sasa kwani ni malengo yetu ambayo tumejiwekea kwa sasa, hakitaeleweka mpaka tubebeb kombe, sapoti kwa mashabiki iendelee," amesema Rashid.

KMC kwa sasa inamsubiri mshindi kati ya Kagera Sugar na Azam FC ambao wanacheza leo ili kumenyana nao hatua ya nusu fainali ya kombe la FA.


Post a Comment

0 Comments