

UONGOZI wa Kagera Sugar umesema kuwa umejipanga kikamilifu kwa ajili ya mchezo wa leo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Azam FC utakaochezwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Kocha mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa wamejipanga kiasi cha kutosha ili kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Azam FC.
"Tumejipanga kikamilifu kupata matokeo chanya mbele ya wapinzani wetu Azam FC, natambua utakuwa mchezo mgumu ila kivyovyote vile lazima tuwakalishe wapinzani wetu kwani tupo tayari kupata matokeo.
"Hakuna timu nyepesi ambayo tunakutana nayo ila kikubwa ni kujipanga na wachezaji nimewapa mbinu mpya ambazo zitatupa matokeo chanya kwenye mchezo wetu, tunahitaji matokeo ili tusonge mbele hatua ya nusu fainali, mpaka fainali hayo ndiyo malengo yetu," amesema Mexime.
Hesabu za Maxime zinagongana na hesabu za kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ambaye naye analihitaji kombe la FA.




0 Comments