Windows

KIONGOZI YANGA AMTAJA ZAHERA KUWA SHINA LA YANGA HIVI SASA


Wakati Yanga ikiendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara na alama 64 kibindoni, aliyekuwa Katibu Mipango wa klabu hiyo, Abdul Sauko, amesema mafanikio hayo yameletwa na Kocha Mwinyi Zahera.

Kiongozi huyo wa zamani Yanga amesema uwepo wa Zahera umewafanya kuwa na furaha wanayanga wote hivi sasa kutokana na mbinu mbalimbali alizokuja nazo Mkongomani huyo.

Sauko ameeleza kama isingekuwa Zahera hivi sasa wangekuwa katika hali ngumu zaidi kulingana na klabu kwa ujumla kukumbwa na hali mbaya kiuchumi.

Amefunguka kuwa Zahera amehamasisha suala la mashabiki na wanachama kuichangia timu ili iwezi kujipatia fedha za kujikimu ikiwemo safari za mikoani na ulipaji wa mishahara.

"Tumepata Kocha ambaye amewafanya Wanayanga kuwa na furaha mpaka leo tupo kileleni mwa msimamo wa ligi.

"Amekuja na ubunifu ambao umesaidia mambo kwenda kama kawaida na kama ingekuwa si yeye tungekuwa pabaya zaidi, amefungua akaunti ambayo wanachama na mashabiki wanachangia, anastahili pongezi" alisema Sauko.

Post a Comment

0 Comments