UONGOZI wa Kagera Sugar, umesema kuwa umeanza kujipanga kwa ajili ya mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya Azam utakaopigwa Aprili 3 Uwanja wa Nyamagana.
Kagera Sugar walipoteza mchezo wao wa hatua ya robo fainali kwa bao 1-0 dhidi ya Azam FC uwanja wa Kaitaba.
Kocha mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa kupoteza mchezo wa kwanza haina maana utapoteza michezo yote kwani mpira una matokeo ya ajabu.
"Kwenye ligi hatupo kwenye nafasi nzuri hivyo nimewaambia vijana wanakazi ya kupambana kupata matokeo chanya, makosa kwenye michezo iliyopita nimeyaona hivyo tumeyafanyia kazi," amesema Maxime.
Kagera Sugar ipo nafasi ya 12 kwenye ligi baada ya kucheza michezo 29 imejikusanyia pointi 36 kibindoni.
0 Comments