Joshua Cheptegei alitawala katika mji wa Aarhus nchini Denmark na kuwa Mganda wa kwanza kushinda ubingwa wa mbio za nyika za dunia sku ya Jumamosi, ikiwa ni miaka miwili baada ya kupoteza mashindano hayo kwenye ardhi ya nyumbani.
Cheptegei aliwaacha hoi Jacob Kiplimo, chipukizi ambaye aliwashangaza wengi kwa kuwachana na mbio za chipukizi ili ashiriki katika mashindano ya wakubwa, na kutwaa ushindi huo.
Mkenya mwngine Geoffrey Kamworor alinyakua shaba. Ni ushindi mkubwa Zaidi wa Cheptegei katika taaluma yake baada ya kutwaa dhahabu mbili katika mashindano ya Jumuiya ya Madola na fedha katika mashindano ya ulimwengu katika mbio za mita 10,000 mwaka wa 2017.
Obiri atamba upande wa wanawake
Katika upande wa wanawake, Mkenya Hellen Obiri alinyakua ushindi wa kihistoria na kuwa mwanariadha wa kwanza wa kike kushinda mashindano ya indoor, outdoor na mataji ya kimataifa. Obiri alimpiku Muethiopia Dera Dida aliyempa ushindani mkali sana. Obiri mwenye umri wa miaka 29, ameongeza taji hilo kwa dhahabu ya mita 5,000 ya London 2012 na mita 3,000 mjini Istanbul 2012. Letesenbet Gidey, Muethiopia mwingine alinyakua shaba.
0 Comments