Windows

Boss wa Simba afunguka kumwachia Ndemla kwenda Yanga





Boss wa Simba afunguka kumwachia Ndemla kwenda Yanga

SIMBA imejibu mapigo kwa Yanga baada ya kuwaambia kiungo wao, Said Ndemla, bado ana mkataba wa miaka miwili kukitumikia kikosi cha Wekundu wa Msimbazi hao hivyo wasijisumbue bure.
Hivi karibuni, Ndemla alienda nchini Sweden kufanya majaribio na amerejea ambapo Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Tena, alitumia mtandao wake wa kijamii kupost picha za kiungo huyo kwa kuandika maneno ya mafumbo hali iliyowafanya baadhi ya mashabiki kudhani Wanajangwani hao wamefika bei.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Crecentius Magori, amefunguka kwamba mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi wasiwe na wasiwasi juu ya kiungo huyo kwani hawezi kwenda kokote kiholela.

“Ndemla yupo Simba, kama Yanga wanahitaji huduma ya kiungo wetu, wanatakiwa kuja tukae mezani tusikilize ofa yao, bado ni kijana wetu kwani ana mkataba,” alisema.

Magori alisema wapo tayari kumuuza kiungo huyo kwenda Yanga endapo uongozi wa Wanajangwani hao watakuwa tayari kununua mkataba wa miaka miwili wa mchezaji huyo.

“Ndemla bado ni mchezaji wetu, kutopata nafasi haimaanishi kwamba hatumhitaji, masuala ya kucheza katika kikosi cha kwanza ni jukumu la Kocha Mkuu Patrick Aussems na tuna imani kwamba atapata nafasi kutokana na falsafa ya mwalimu,” alisema Magori.

Post a Comment

0 Comments