BARCELONA imepanga kumtoa chambo Philipo Countinho au Malcom kwenda Manchester United ili wao wapate saini ya mshambuliaji Marcus Rashford.
Taarifa zimeeleza kuwa kutokana na Man United kuhitaji saini ya Coutinho imesababisha Barcelona kumtumia kiungo huyo wa zamani wa Liverpool au Malcom ili iwe rahissi kumnasa Rashford.
Mbali na Rashford, Barcelona inaendelea kumsaka mshambuliaji ambaye itakuwa naye muda mrefu na macho yao yapo kwa Antoine Griezmann na Luka Juvic.
Barcelona ni vinara wa La Liga wakiwa na pointi 66 baada ya kucheza michezo 28.
0 Comments