

Wakati kikosi cha Simba kikiendelea kula viporo vyake, uongozi wa timu hiyo umesema malengo yake ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa misimu 10 ijayo mfululizo.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameeleza kwa kikosi walichonacho hivi sasa kinawapa jeuri hiyo.
Manara ameeleza kuwa wanataka kuifikia na ikiwezekana kuizidi mataji Yanga ambayo imetwaa mara 27 huku Simba wakiwa wamechukua mara 18 tu.
Simba wikiendi hii itakuwa na kibarua kingine cha ligi mjini Shinyanga na kuelekea mechi hiyo Manara amesema wamejipanga vizuri.
Tayari kikosi kipo njiani na Kocha Mkuu, Mbelgiji Patrick Aussems amesema wanaenda kupigania alama tatu muhimu kujiwekea mazingira mazuri ya kuchukua ubingwa.




0 Comments