

Kocha wa klabu ya Stand United, Athuman Bilal 'Bilo', amesema mechi yao ijayo dhidi ya Simba ni ya kawaida mno.
Simba na Stand zitakutana tena katika mchezo ambao utakuwa ni wa raundi ya pili ambapo Stand wakiwa na kumbukumbu ya kichapo cha mabao 3-0 kwenye Uwanja wa taifa.
Bilo ametamba kuwa mechi dhidi ya Simba ni ya kawaida sana kama wanacheza na Lipuli, Ndanda, Singida United na timu zingine.
Ameeleza kuiona Simba kama timu zingine akisema ina kikosi cha kawaida hivyo hawana presha kabisa kuelekea mechi hiyo.
"Simba ni wa kawaida mno, sioni utofauti na timu zingine, tutawashangaza kama ilivyokuwa kwa Yanga wakija Shinyanga" alisema.




0 Comments