Windows

TANZIA: RAPA ZILLA AACHA PENGO KWENYE TASINIA YA BONGO FLEVA


TANZIA: Tasnia ya Bongo Fleva imepata pigo baada kuondokewa na Rapa maarufu Goldeb Jacob Mbunda 'Godzilla'nchini, ambaye amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo Jumatano, Februari 13, 2019 akiwa nyumbani kwao, maeneo ya Mbezi Salasala Dar es Salaam.

Mwili wa marehemu umepelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam na msiba upo nyumbani kwao Salasala.

Taarifa za awali zimedai kuwa kabla ya kufika na umauti, Godzilla alikuwa akisumbuliwa na tumbo, presha na kisukari.

Alizaliwa Januari 5, 1988 mkoani Morogoro na alikuwa Rapa aliyetikisa Bongo kwa ngoma zake Get High, King Zilla, Milele aliyomshirikisha Kiba, First Class akiyokuwa na Mwasiti.


Post a Comment

0 Comments