

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, ametangaza kuwoanea huruma Yanga kuelekea mchezo dhidi ya Simba Jumamosi ya wiki hii.
Huruma hiyo imekuja kutokana na kipigo walichokitoa jana Simba dhidi ya al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliomalizika kwa ushindi wa bao 1-0.
Rage ameeleza kuwa anawaonea huruma Yanga ukizingatia Simba hivi sasa imekuwa ni bora zaidi ya Yanga kwa kitakwimu.
Amesema kuwa kwa sasa Yanga ni timu ambayo ni ya kawaida na anapendelea kuona ikifungwa mabao 6-0 ili kuweka heshima nzuri mjini.
"Nawaonea huruma watani zetu kwani Simba ya sasa ipo vizuri, ningependa kuona walau wanafungwa bao 6 pekee ili kuweka heshima hapa mjini" alisema.
Timu hizo zenye historia ya aina yake haswa katika soka la Tanzania zitakuwa zinakutana wikiendi ijayo huku katika mechi iliyopita zilishindwa kufungana kwa kwenda suluhu tasa.




0 Comments