Timu ya Tanzania imepangwa kucheza na timu ya Sudan katika hatua ya awali ya kufuzu michuano ya CHAN michuano ambayo itafanyika mwaka 2020 huko nchini Ethiopia.
Michuano hiyo huhusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya nchi na Tanzania itaanza na Sudan na baada ya hapo ikufuzu itakutana na mshindi kati ya Kenya na Burundi.
Mshindi wa hapo atakuwa amefuzu moja kwa moja kushiriki michuano hiyo, Sudan walikuwa washindi wa tatu katika michuano iliyopita ikifanyika nchini Kenya michuano ambayo bingwa alikuwa Morocco.
0 Comments