Windows

Ratiba Ligi kuu TPL leo 1 February 2019

Ligi kuu soka ya Tanzania bara itaendelea leo kwa jumla ya mechi nne kuchezwa katika viwanja mbalimbali.
Katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kutakuwa na mechi kati ya Kagera Sugar dhidi ya Tanzania Priosns saa kumi kamili jioni.
Nako mkoani Shinyanga dimba la Kambarage chama la wana watakuwa wenyeji wa KMC kuanzia saa kumi kamili jioni.
Nako katika uwanja wa Meja Jenarali Isamuhyo huko Mbweni jijini Dar Es Salaam maafande wa JKT Tanzania watakuwa nyumbani kuwakaribisha Mwadui kutoka Mkoani Shinyanga.
Ruvu Shooting wazee wa kupapasa watakuwa wenyeji wa Mbeya City uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani.

Post a Comment

0 Comments