Windows

SIMBA YATANGAZA VITA KUPAMBANA NA 'MAJAMBAZI' HAWA WANAOWAKWAMISHA



UONGOZI wa Simba umesema kuwa kuna watu wajanja ambao ni 'majambazi' na wanafanya mambo kinyume n utaratibu kwa kutoa fomu za uanachama wa klabu ya Simba.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa watu hao hutoa pia kadi za uanachamana wana mihuri kabisa ya klabu ambayo ni feki wanaitumia kuhalalisha uovu wao wanaoufanya.

"Wanachokifanya hicho watu ni wizi na utapeli na kwa sasa klabu yetu imesitisha kabisa utoaji wa kadi za uanachama mpaka pale tutakapotoa taarifa rasmi juu ya upatikanaji wa wanachama wapya hivi karibuni ambao watakuwa wanahisa wapya.

"Ikitokea kiongozi yoyote ama mwanachama yeyote akapatikana anafanya 'ujambazi' huu itolewa taarifa kwenye kituo chochote cha polisi kilicho karibu au klabuni Msimbazi," amesema Manara.

Post a Comment

0 Comments