Windows

MENEJA SARRI AMKINGIA KIFUA MLINDA MLANGO WAKE



MENEJA wa Chelsea, Maurizio Sarre amesema kuwa kitendo cha mlinda mlango wake Kepa Arrizabalaga kugoma kufanyiwa mabadiliko ilikuwa ni nia ya kuendelea kuitetea timu yake kwani aliamua kufanya hivyo akidhani mchezaji wake ameumia.

Kwenye mchezo huo wa kombe la Carabao lililobebwa na Manchester City kwa mikwaju ya penalti 4-3 na kufanya iwe mara ya sita kwao kulibeba kombe hilo.

"Wachezji wangu walicheza kwa juhudi na walionyesha kwamba wanapambana kwa ajili ya kutafua matokeo, ila Kepa aliona bado ana nafasi ya kutetea timu yake hivyo nitakaa naye kuzungumza kuhusu mwenendo wake ili awe katika ubora wake zaidi," amesema.

Kepa naye amesema alishindwa kutoka kwa kuwa alikuwa hajaumia bali alikuwa anajaribu kupoteza muda na kushusha presha kwa wachezaji wake ambao walikuwa wanashambuliwa hasa dakika za lala salama.

Post a Comment

0 Comments