

UNAKUMBUKA ile kauli ya uongozi wa Simba kupitia kwa ofisa habari wao, Haji Manara kwamba kuna watu wamewashikia nafasi ya kwanza kwa muda kisha watairudisha wakati ukifika? Basi leo Ofisa Habari wa Yanga naye amekuja kivingine na kusema msimu huu wanahitaji kuchukua ubingwa wao ambao kuna timu wameikopesha.
Ten amesema kuwa baada ya kurejea kutoka Lindi wakiwa wamebeba ushindi mbele ya Namungo FC sasa hesabu zao ni kufanya vema kwenye mechi zao za ligi zinazofuata.
"Hesabu zetu kwa sasa ni kuona tunaendelea kubeba pointi tatu kwenye michezo yetu inayofuata ambapo tutaanza na Alliance FC mchezo utakaochezwa uwanja wa CCM Kirumba, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao.
"Mpira ni mashabiki uwepo wao kwetu ni faraja, tunahitaji kuchukua ubingwa msimu huu ambao kuna watu tuliwakopesha, tunajua hilo linawezekana na kazi inaendelea," amesema Ten.




0 Comments