Windows

SINGIDA UNITED WAMREJESHA KUNDINI KOCHA WALIYEMTEMA


Uongozi wa Singida United umeamua kumuita tena Kocha Fredrick Minziro kwa ajili ya kuhudumu ili kuongeza nguvu katika benchi la ufundi ndani ya kikosi chao. Imeelezwa.

Minziro amerejea tena Singida United ikiwa ni baada ya kuondoshwa kipindi alipoifanikisha kupanda daraja mpaka Ligi Kuu Bara mwaka 2017.

Licha ya kumfukuza kipindi kile, Singida wameona isiwe tabu kumrejesha Minziro ambaye wanaamini atalisaidia benchi la ufundi kuendeleaza harakati za kufanya vizuri katika ligi.

Wakati kikosi cha Singida United kinaendelea kujifua kujiandaa na mechi za ligi zilizopo mbele yao.

Walima alizeti hao bado wanaugulia maumivu ya kupigwa 2-0 na Ndanda FC katika mchezo uliopita huko Nagwanda Sijaona, Mtwara.

Post a Comment

0 Comments