Windows

Simba : Mastraika 2 walioanza dhidi ya Yanga kuwakosa African Lyon

Simba : Mastraika 2 walioanza dhidi ya Yanga kuwakosa African Lyon
Baada ya kuwakalisha Watani wao wa Jadi Jumamosi ya wiki iliyopita kwa kuwafunga bao 1 kwa 0 kwenye mchezo wa ligi kuu soka ya Tanzania bara Simba leo itakuwa uwanjani jijini Arusha kucheza na African Lyon.
Simba itawakosa washambuliaji wake wawili ambao walianza katika mchezo kati ya Yanga na Simba uliochezwa jumamosi kutokana na washambuliaji hao kuwa na kadi tatu za Njano.
Wachezaji hao ni Meddie Kagere raia wa Rwanda na Emmanuel Okwi raia wa Uganda katika mchezo huo utakaoanza saa kumi kamili uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Post a Comment

0 Comments