Windows

SIMBA: HAMNA NAMNA LAZIMA TUTOKE TU KWA LIPULI LEO


LEO Simba watakuwa kibaruani kumenyana na Lipuli FC ukiwa ni mchezo wa ligi kuu utakaochezwa uwanja wa Samora.

Lipuli tangu wapande ligi msimu wa 2017/18 hawajaruhusu ushindi wala hawajaonja ushindi mbele ya Simba licha ya kukutana mara tatu.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema anatambua ugumu wa mchezo huo ila wamejipanga kuona wanapata matokeo mbele ya wapinzani wao Lipuli.

"Tumekutana nao mara tatu mpaka sasa hakuna ambaye ameweza kuibuka na ushindi hivyo utakuwa ni mchezo mgumu na unachangamoto kubwa kwetu.

"Kocha wa Lipuli Seleman Matola aliwahi kuwa mchezaji wa Simba hivyo anatujua vizuri namna tulivyo ila hamna namna ni suala la muda tu," amesema Manara.


Post a Comment

0 Comments