

Kipa wa Yanga, Klaus Kindoki, ameibuka na kusema kuwa bado kiwango chake hakijarudi vema na akiwataka mashabiki waache kumsifia mapema.
Kipa huyo kutoka Congo ameeleza kuwa kwa sasa ndiyo ameanza kurejesha kiwango chake taratibu lakini hajawa namna vile anavyojijua.
Amesema hapo awali alikuwa anapatwa na wakati mgumu juu ya kuelewana na wenzake uwanjani sababu ya lugha ya Kiswahili lakini kwa sasa mambo yanaenda FRESH.
Baada ya mchezo dhidi ya Namungo, Kindoki amesema ataendelea kupambana kwa juhudi zote ili kuhakikisha anarudisha kiwango chake kwa asilimia 100.
Wakati huo kikosi cha Yanga hivi sasa kiko katika maandalizi moto ya kucheza dhidi ya Alliance, mechi ambayo inafuata kwao kwenye Ligi Kuu Bara.




0 Comments