

KOCHA wa Lipuli FC, Seleman Matola amesema kuwa ana hamu ya kuwa wa kwanza kuwanyoosha wapinzani wake Simba leo kwenye mchezo wao wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Samora.
Simba wamekuwa wakipata taabu sana kuinyoosha Lipuli tangu msimu wa mwaka 2017/18 na leo wanakutana mara ya nne huku Lipuli wakipania kubeba pointi tatu.
Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa wamekutana na Simba mara tatu na katika michezo hiyo hakuna aliyebahatika kuibuka na ushindi zaidi ya kubeba pointi moja hivyo wamejiandaa kuvunja mwiko huo.
"Unajua wapinzani wetu wapo vizuri ukizingatia matokeo yao yamekuwa chanya kwenye mechi zao, sasa hapo ndipo tunapataka tutibue furaha yao tuwe wa kwanza kubeba pointi tatu hapa nyumbani, madhaifu yao tunayajua tutawanyoosha mapema tu," amesema Matola.
Mchezo wa kwanza walipokutana Samora, walitoka sare ya kufungana bao 1-1 na mchezo wa marudiano Uwanja wa Taifa, walifungana bao 1-1 na mchezo wa msimu huu walitoka suluhu Uwanja wa Taifa.




0 Comments