Windows

KOCHA WA AZAM FC AANZA KWA USHINDI BILA YA UWEPO WA PLUIJM KWENYE BENCHI



KOCHA Mkuu wa Azam FC, Abdul Mingange jana ameongoza kikosi chake kwa mara ya kwanza na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Rhino Rangers kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho.

Mingange ametwaa mikoba ya aliyekuwa kocha mkuu Hans Pluijm na msaidizi wake Juma Mwambusi baada ya uongozi kuamua kuwatimua kwa kile walichoeleza ni matokeo mabaya ya Ligi Kuu Bara.

Mabao ya Azam FC yalifungwa na Tafadzwa Kutinyu aliyecheka na nyavu mara mbili ikiwa ni dakika ya 21 na 54 huku bao la tatu likiwekwa kimiani na Obrey Chirwa dakika ya 69.

Kwa matokeo hayo Azam FC wanatinga hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho ambalo kwa sasa halina bingwa mtetezi kwani Mtibwa Sugar alivuliwa ubingwa na KMC. 

Post a Comment

0 Comments