

Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake mjini Morogoro kuwawinda mabingwa wa Tanzania, Simba.
Yanga inashuka dimbani mechi ijayo dhidi ya watani wake Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi.
Tokea kikosi hicho kimetua mjini Morogoro kutoka yanga, Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera amekuwa akifanya kazi ya ushambulizi.
Zahera amekuwa akiwanoa washambulizi wake kwa njia mbalimbali.
Mazoezi ya kwanza waliyofanya aliendelea kuboresha mbinu za ufungaji.
Zahera amekuwa akifanya hivyo kuhakikisha viungo na hata walinzi wakisaidia wakati wa ushambulizi.
Yanga ndio vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 58 baada ya mechi 23.




0 Comments