Windows

MATOKEO YA SIMBA NA YANGA YAMPA KIGUGUMIZI KOCHA BONGO


KOCHA wa timu ya Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa ni ngumu kutabiri mshindi wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga utakaochezwa Februari 16 Uwanja wa Taifa.

Kwenye mchezo wa kwanza wa msimu huu ambao Simba alikuwa mwenyeji na matokeo yake yalikuwa suluhu huku bingwa wa mchezo akiwa ni mlinda mlango Beno Kakolanya watakutana jumamosi huku Beno akiwa yupo nje ya timu ya Yanga.

"Hakuna wepesi kwa timu hizi zinapokutana uwanjani kutokana na ushindani wake uliopo, dakika tisini ndiyo zitaamua nani atakuwa mshindi katika mchezo wao.

"Kwa timu ambayo itakuwa makini kutumia makosa ya mpinzani wake ndiyo itapata nafasi ya kupata matokeo katika mchezo wao," amesema Matola.


Post a Comment

0 Comments