

KOCHA mkuu wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa mzunguko wa pili anapata taabu kupata ushindi kutokana na kucheza na zaidi ya timu moja akiwa Uwanjani.
Zahera alianza kupoteza mchezo wake wa kwanza mbele ya Stand United ikiwa ni mchezo wake wa 20 kwani aliongoza timu kucheza michezo 19 bila kupoteza.
Zahera amesema wapinzani wao wanacheza mechi zao kwa kutoa ahadi ya fedha kwa wachezaji ili washinde hali ambayo inamfanya awe kwenye wakati mgumu.
"Nashindwa kupata matokeo chanya uwanjani, nacheza na timu zaidi ya moja uwanjani hali ambayo inafanya ushindani uwe mkubwa.
"Licha ya yote hayo nashukuru wachezaji wangu wanajituma na ninapata matokeo, ukweli ni kwamba kuna watu wanacheza mechi zetu na wanapaswa wajue kwamba hakuna siri ya watu zaidi ya wawili," amesema Zahera.
Zahera alipoteza pointi mbili mbele ya Coasatal Union kisha akapoteza nyingine mbele ya Singida United kabla ya kuibukia tena Mkwakwani na kubeba pointi tatu mbele ya JKT Tanzania.



0 Comments