Windows

KAGERE AFICHUA KILICHO NYUMA YA BAO LAKE KWA WAARABU


MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere amesema kuwa kikubwa kinachoibeba timu yake ya Simba ni ushirikiano pamoja na maombi.

Kagere jana alifunga bao dakika ya 64 akitumia pasi matata ya nahodha John Bocco ambalo limeifanya Simba kuketi kiti cha nafasi ya pili kwenye Ligi ya Mabingwa Afika kikiwa na pointi sita huku kinara akiwa ni Al Ahly ya Misri.

"Ni furaha kwa timu na tunaona fahari kupata ushindi ambao ni muhimu kwetu na mashabiki wetu, ugumu uliopo ni changamoto kwetu tunaendelea kupambana kikubwa ni maombi na juhudi," amesema.

Kwenye kundi D ambalo wapo Simba walianza kwa ushindi mbele ya JS Saoura kisha wakaambulia kipigo mara mbili kwa AS Vita na Al Ahly kwa kukusanya mabao 10, ushindi wa jana umeamsha morali kwa wachezaji na mashabiki.

Post a Comment

0 Comments