Windows

YANGA YAPATA MCHECHETO NA SIMBA, YAFUNGUKA ITAKACHOWAFANYA TAIFA


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera amesema kuwa kikosi chake hakina hofu ya kupoteza mbele ya Simba kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Jumamosi Uwanja wa Taifa.

Zahera amesema ushindi wao wa jana dhidi ya Al Ahly hamsumbui kwani anaamini utawaponza Simba wataingia uwanjani kifua mbele hapo ndipo watakutana na kichapo cha aina yake.

"Najua wameshinda na wana furahia hilo kwa sababu niliwaona wakiwa kazini nawatambua hawanisumbui, nimewaamba wachezaji wangu wasiwe na presha waingie uwanjani wakijiamni tutapata matokeo.

"Kama nitafungwa ni sawa kama nitafunga pia nitafurahi kwa kuwa nimejiaanda na natambua mpira una matokeo ya ajabu sina mashaka na kikosi changu," amesema Zahera.

Yanga itaikaribisha Simba kwenye mchezo wao wa ligi ikiwa ni marudio wakiwa na kumbukumbu ya kutoka suluhu kwenye mchezo wao wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Taifa.

Post a Comment

0 Comments