Windows

AKILI ZA KOCHA WA TIMU YA TAIFA IPO KOMBE LA DUNIA KWA SASA


ZIKIWA zimebaki siku 72 kuanza kwa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 ambayo itafanyika hapa nchini kocha mkuu Oscar Mirambo amebainisha malengo yake makubwa.

Mashindano hayo ambayo yanashirikisha timu nane ambazo ni Tanzania, Nigeria, Angola na Uganda ambao ni kundi A pamoja na Guinea, Cameroon, Morocco na Senegal ambao ni kundi B inatarajiwa kuanza Aprili 14 hadi 28 mwaka huu.

Mirambo amesema kufanyika nyumbani mashindano hayo ni fursa pekee kwa Tanzania kuitumia vema na itakuwa ni njia pekee ya kujitathimini kutokana na yale ya kushiriki awali ambayo yalifanyika nchini Gabon mwaka 2017.

"Mipango ambayo ipo kwa sasa ni kuona timu yetu inafanikiwa kushiriki michuano ya kombe la Dunia itakayochezwa hapo baadaye nchini Peru ambapo ni mpango wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pamoja na Serikali kwa ujumla.

"Michuano ya mwaka 2017 tuliishia hatua ya makundi kwa sasa tunahitaji kusonga mbele zaidi ya mwanzo kwa kutumia faida ya uwanja wa nyumbani," alisema Mirambo.


Post a Comment

0 Comments