Nahodha wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajibu amesema kuwa wachezaji wote wana morali na hitaji lao kubwa ni kucheza michezo mitatu kwenye kombe la SportPesa Cup ambalo linaanza leo Uwanja wa Taifa.
Michuano ya SportPesa inashirikisha timu nane ikiwa ni nne kutoka Kenya ambazo ni Gor Mahia, KK Sharks, Bandari na AFC Leopards na nne kutoka Tanzania ambazo ni Simba, Yanga, Mbao na Singida United.
"Wachezaji wanatambua kazi kubwa ambayo ipo mbele yetu na malengo yetu makubwa ni kufanikiwa kucheza mechi tatu kwenye michuano hii ya SportPesa Cup ambayo ni hii ya robo fainali ya leo, nusu fainali pamoja na mchezo wa fainali," alisema Ajibu.
Mchezo wa kwanza leo utakuwa kati ya Singida United na Bandari ukifuatiwa na mchezo wa Yanga na KK Sharks huku kiingilio kikiwa ni Sh 2,000 VIP B na C 5,000 na VIP A 10,000.
0 Comments