Baada ya hapo jana Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad
kuhojiwa na Kamati ya Haki,Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge kufuatia kauli za kudhalilisha
Bunge, leo ni zamu ya Mbunge wa Kawe Halima Mdee.
Utambuka January 7 mwaka huu Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza na waandishi wa habari alimtaka Halima Mdee kufika kwenye kamati hiyo siku ya leo.
Tayari Halima alishaeleza kuitika wito huo wa kufika mbele ya kamati kama alivyotakiwa. si mara ya kwanza kwa Mbunge huyo kuhojiwa na kamati hiyo.
0 Comments