Windows

VIFAA VIWILI VYAONGEZWA YANGA KUENDELEZA MAKALI KIKOSINI, KOMBE LA FA NDANI


Zikiwa zimesalia siku chache kuelekea mechi ya Kombe la FA dhidi ya Yanga na Biashara, uongozi wa Yanga umesema wachezaji wake, Juma Mahadhi na Rafael Daud wamerejea kikosini.

Wawili hao walikuwa majeruhi kwa muda mrefu haswa Mahadhi na kupelekea kuwa nje ya kikosi cha Yanga kwa muda mrefu.

Yanga itakuwa inaenda kucheza na Biashara tarehe 31 mwezi huu huku Kocha Mkuu wa timu, Mwinyi Zahera akisema ni moja kati ya malengo yake kutwaa ubingwa huo.

Kuna uwezekano wachezaji hao wakawa sehemu ya kikosi cha Yanga ambapo kimekuwa kikipambana kwa hali na mali licha ya kuwepo kwa changamoto ya kuyumba kwa uchumi.

Ujio wa Mahadhi na Daud unaweza kuongeza chachu ya upana wa kikosi cha Yanga ambacho pia katika ligi kimeshika namba moja kileleni.

Post a Comment

0 Comments