Windows

SALAAM KWA WATANI ZAANZA, ZAHERA AONGEZA MASHINE MBILI TAYARI KUWAUA SIMBA


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameanza kutuma salaam kwa watani zake wa jadi Simba kuelekea mechi ya mzunguko wa pili katika Ligi Kuu Bara.

Zahera amekiri kuwa Simba wapo vizuri lakini hawana sababu ya kuwachukulia poa Yanga ambao wana kikosi cha kawaida.

Kocha huyo kutoka Congo, ametamba kuwa katika kikosi chake atakuwepo mchezaji Mohammed Issa Banka ambaye alifungiwa kutokana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni.

Ujio wa Banka umemfanya Zahera awataje Simba kuwa wajiandae maaana kikosi chake kitakuwa cha moto.

Aidha, Zahera amemtaja mchezaji Gustavo kutoka Yanga B kuwa ni kifaa hatari na anaweza akampa nafasi ya kucheza siku hiyo.

Timu hizo zitaenda kukutana zikiwa na kumbukumbu ya kwenda suluhu ya kutofungana katika mkondo wa kwanza wa ligi.

Post a Comment

0 Comments