Taarifa zinaeleza mpaka sasa haijajulikana ni lini utafanyika kufuatia ukimya ambao upo na inasemekana wanachama waliofungua kesi mahakamani hawajafuta kesi zao.
Wanachama baadhi walifungua kesi kupinga kufanyika kufanyika kwa uchaguzi huo na lakini baadaye baadhi ya viongozi Yanga waliwashawishi kuzifuta japo imekuwa ngumu.
Hivi karibuni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Ally Mchungahela, alisema wanazungumza vema na wanachama hao kuhakikisha wanafuta kesi zao na akaeleza maendeleo ni mazuri.
Uchaguzi wa Yanga ulipaswa kufanyika tarehe 13 mwezi huu wa kwanza lakini mpaka sasa umeshindika na leo ikiwa ni tarehe 29 kuelekea mwisho wa mwezi bado haijajulikana hatma ni nini.
0 Comments