Windows

VIDEO: MAKONDA AWAPIGWA MKWARA WASANII, JB


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, jana Januari 31, amekutana na wasanii kutoka katika tasnia zote nchini ikiwemo Muvi, Bongo Fleva, Muziki wa asili, wacheza mpira, kwa ajili ya kujadili kwa pamoja masuala mbalimbali yanayohusu sanaa nchini. Mkutano huo unafanyika katika ukumbi wa Leaders Club Kinondoni jijini Dar.

Akizungumza katika kikao hicho, RC Makonda amesema ni mkutano wa wazi ambao wasanii wote walipaswa kutoa mawazo yao ili Serikali imeze kuwasaidia na ambaye anataka mkutano wa privacy kama alivyoomba msanii JB, basi akafanye mkutano wake au akazungumze na mkewe kwani kinachojadiriwa hakina usiri wowote.

Awali, JB alimwomba mkuu huyo wa mkoa kuunda kamati maalum kwa ajili ya kwenda kujadili kwa kina yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye mkutanio huo akidai kuna baadhi ya vitu haviwezi kusemwa hadharani.


Post a Comment

0 Comments