Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion na muandaaji wa Tamasha la Pasaka na Bw. Alex Msama amesema kuwa wamepokea maelekezo kutoka Baraza la Sanaa nchini (BASATA) likiwataka wasanii wa muziki wa injili watakaoshiriki katika tamasha hilo kujisajili BASATA ikiwa ni kutekeleza matakwa ya sheria na kanuni za baraza hilo
Msama ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari wa mitandao mbalimbali ya kijamii pamoja na vyombo vingine vya habari ofisini kwake Kinondoni jijini Dar es salaam.
Amesema Baraza la sanaa limewataka wasanii wote watakaotumbuiza kwenye tamasha la Pasaka kujisajili kwenye baraza hilo kwa wakati ili kutimiza vigezo vya ushiriki wao.
Msama ameongeza kuwa wasanii ambao bado hawajajisajili basata wafanye hivyo ili waweze kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye tamasha hilo litakalofanyika Aprili 21 jijini Dar es Salaam
Amesema Basata wametoa agizo hilo kwa mujibu wa sheria suala la kujisajili ni la lazima, hivyo akasema wasanii wote wanatakiwa kupewa vibali ili waweze kutambulika mahali popote wanapokwenda.
Amesema wasanii wengi wamekuwa wakiipuuza Basata lakini baraza hilo linaumuhimu mkubwa katika kulinda maslahi ya wasanii.
Akizungumzia faida za kujisajili, Msama amesema ni pamoja na kufuata sheria na taratibu za nchi, kutambuliwa na serikali, kupata utambulisho wa Baraza katika mahitaji mbalimbali, fursa za kushiriki maonesho, taifa kuwa na takwimu sahihi za wadau wanaojihusisha na shughuli za sanaa na faida nyingine.
Katika hatua nyingine, Msama alisema wapo kwenye mazungumzo na wasanii mbali mbali wa nje kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tamasha hilo linalofanyika kila mwaka na kwamba asilimia 80 ya wasanii hao wataimba kwa kutumia vyombo ‘live’ sio CD.
0 Comments