Windows

AKILIMALI ATOA TAMKO TENA YANGA, AITAJA SIMBA


Mjumbe wa Baraza la Wazee katika klabu ya Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, ameipa nafasi kubwa Yanga ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu bara msimu huu.

Akilimali amefunguka kwa kujiamini kwamba Yanga ina nafasi hiyo licha ya kuwa ipo kwenye kipindi cha mpito wa fedha ikiyumba kiuchumi.

Mzee huyo ambaye amekuwa akipokea lawama kubwa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo juu ya mabadiliko ya Yanga, ameeleza kuwa kikosi cha Yanga kipo imara kwa sasa.

Amesema Simba imeshapata ubingwa wa pesa pekee lakini uwanjani haitaweza kuonesha maajabu yoyote yale ambayo yataweza kuipa manufaa katika kuwania ubingwa.

"Simba wale wana ubingwa wa fedha tu, lakini tukija uwanjani sisi ndiyo tutakitwaa kikombe cha ligi kuu bila tatizo lolote" alisema.

Kikosi cha Yanga hivi sasa kipo katika maandalizi ya kucheza na Biashara ya Mara katika mchezo wa Kombe la FA Jumamosi ya wiki hii.

Post a Comment

0 Comments