Mshambuliaji Sadney Urikhob aliyekuja kwa majaribio Simba ameondoka nchini kurejea kwao Namibia.
Urikhob alikuja nchini kufanya majaribio hayo huku kocha Patrick Aussems akiwa ameonyesha kuridhishwa na kiwango chake.
Imeelezwa sraika huyo alitua nchini akitokea Indonesia na alicheza mechi 2 za michuano ya Sportpesa Cup.
Taarifa imesema Kocha Aussems ameahidi kushughulikia suala lake baada ya mechi ya dhidi ya Al Ahly huku Hunlede Kisimbo amefeli majaribio.
Taarifa za chini ya kapeti zinasema Mnamibia huyo akisharejea na mipango ya Aussems kishafanikisha juu ya usajili wake anaweza akasini mkataba wa mwaka mmoja au miwili.
0 Comments