Windows

KAKOLANYA AFUNGUKA UPYA JUU YA SUALA LAKE NA YANGA


Baada ya kuomba kuvunjiwa mkataba wake na uongozi wa klabu ya Yanga, mlinda mlango, Beno Kakolanya, amesema hawezi kuzungumza lolote kwa sasa bali anamwachia Wakili wake.

Kakolanya ambaye alitua Yanga akitokea Tanzania Prisons, amesema tayari Wakili wake ameshakamilisha kupeleka barua Yanga na kilichobaki kitasimamiwa na Mwanasheria huyo.

Kakolanya na Wakala wake waliamua kukaa chini na kuamua kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba kutokana na timu yake kushindwa kumlipa stahiki ikiwemo mshahara.

Tayari Yanga imekiri kupokea barua hiyo ambayo wamesema nao wataijibu kisheria, ambapo wamemtaka Kakolanya na Wakili wake wasubirie majibu hayo ya kisheria.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti, Samuel Lukumay, amefunguka kwa kukiri kuipokea barua hiyo ambayo wataitolea majibu siku yoyote kuanzia leo.

Post a Comment

0 Comments